Wednesday, June 27, 2012

Mahakama ya Misri yabatilisha sheria

Mahakama nchini Misri imebatilisha uamuzi wa serikali uliowaruhusu polisi kuwakamata raia.
Serikali ya mpito ya nchi hiyo iliianzisha sheria hiyo mapema mwezi huu wakati uchaguzi wa urais ulipokuwa ukikaribia.
 Sheria hiyo ilipingwa vikali na makundi ya kutetea haki za binaadamu na wanasiasa, wakilishutumu jeshi kwa kujaribu kuirejesha tena sheria ya utawala wa hali ya hatari ambayo muda wake ulimalizika wiki mbili zilizopita.

Sheria hiyo iliwapa maafisa wa jeshi la polisi mamlaka makubwa ya kuwakamata raia, hali ambayo inaonekana kuwa na mchango mkubwa katika mapinduzi dhidi ya aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak.

 Uamuzi huo wa mahakama ni pigo kubwa kwa utawala wa kijeshi unaojiandaa kukabidhi madaraka kwa rais mpya, Mohammed Mursi.

No comments:

Post a Comment