Mmoja
wa Waratibu wa maandalizi ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 (pili
kulia) Sebastian Maganga akifafanua baadhi mambo mbele ya wageni
waalikwa wakiwamo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakati wa uzinduzi
rasmi wa tamasha hilo uliofanyika kwenye viwanja vya Lidaz
Club,Kinodoni jijini Dar leo,tamasha hilo linatarajia kutimua vumbi zake
hivi karibuni katika mikoa mbalimbali,ambapo katika tamasha hilo
mdhamini mkuu ni kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake Serengeti
Premium Lager,Kampuni ya mafuta ya Gapco pamoja na Push Mobile.Kauli
mbiu ya tamasha hilo ni "MUONEKANO MPYA-BURUDANI ILELE-BAAAS"!
Sehemu
ya zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta
2012,ikiwemo Magari aina ya Toyota Vitz kila moja yenye thamani ya
shilingi milioni nane,Piki piki a.k.a Boda Boda 14 kila moja ikiwa na
thamani ya shilingi milioni moja na nus na zawadi nyingine zikiwemo simu
aina ya blackberry,Nokia.
Baadhi
ya Wadau mbalimbali wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishuhudia
uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya lidaz Club,jijini dar.
Mmoja
wa waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Sebastian Maganga
akifafanua jambo kwa umakini na kuweka misisitizo kwa Wanahabari
waliofika kwenye uzinduzi wa tamasha hilo.
Sebastian
Maganga kutoka Clouds Media Group akiwatambulisha Wadhamini wa tamasha
la Serengeti Fiesta 2012,Kutoka kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya
mafuta ya Gapco,Ben Temu,Meneja wa kinywaji cha Serengeti kutoka
SBL,Allan Chonjo pamoja na muwakilishi wa kampuni ya Push
Mobile,Bw.Rodney
Meneja
wa bia ya Serengeti kutoka kampuni ya SBL,ambao ndio wadhamini wakuu wa
tamasha la Fiesta 2012,Allan Chonjo akizungumza machache mbele ya
wageni waalikwa wakiwemo wanahabari kutoka vyombo
mbalimbali,uliofanyika leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,jijin Dar.
Bw.Rodney
ambaye ni muwakilishi wa kampuni ya Push Mobile akionesha moja ya namba
zitakazotumika kutoa taarifa mbalimbali za tamasha hilo litakaloanza
kutimua vumbi zake kuanzia hapo kesho katika mikoa ya Arusha na Mbeya na
baadaye mikoa mingine.
Pichani
shoto ni Meneja mahusiano ya ndani ya kampuni ya bia ya
Serengeti,Bw.Iman Lwinga akiwa sambamba na baadhi ya wanahabari
waliofika kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Wageni
waalikwa wakiwemo wasanii kadhaa bia walifika kushudia tukio hilo kubwa
la kihistoria katiak tasnia ya burudani hapa nchini.
Wakifuatilia kwa umakini zaidi.
Kwa mshangao mkubwa wakishuhudia uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Lidaz Club.
Wadau wakifuatilia uzinduzi huo,akiwemo Shaffih Dauda mzee wa sports bar.
Meneja
wa vinywaji vikali wa SBL,Bw.Emillian Rwejuna akizungumza na Meneja wea
kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Allan Chonjo wakati wa uzinduzi wa
tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mtangazaji
wa Clouds FM,Millard Ayo akifanya mahojiano mafupi na msanii wa muziki
wa kizazi kipya,Mwasiti kuhusiana na tamasha la fiesta kwa ujmla.
Wadadazi nao walikuwepo kunogesha uzinduzi huo wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
No comments:
Post a Comment