Dk.
Cathbert Mchalo wa Taasisi ya Mifupa ya Moi (kushoto), akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kumpokea, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Madaktari Tanzania kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha
aliyopata kutokana na kipigo.
Ofisa
wa Polisi akimzuia mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima, Francis
Dande, asimpige picha wakati wakimuondoa askari mwenzao aliyeshambuliwa
na madaktari akituhumiwa kukutwa akipiga simu ya kuwataarifu wenzake
kuwa Dk. Ulimboka hakufa.
Mmoja
wa wana usalama wa (wa pili ushoto), akizozana na madaktari baada ya
kumbaini akijifanya ni mwandishi wa habari na kumuamuru kuondoka eneo
hilo mara moja.
Mmoja
wa madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wa pili kulia,
akizozana na Askari Polisi waliofika hospitalini hapo wakidai
wanatafuta redio yao ya mawasiliano iliyopotea wakati wa pilikapilika
za kumpokea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa
madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, alipoletwa akiwa hoi kutokana na
kipigo kutoka kwa watu waliomteka usiku wa kuamkia jana na kumtupa
msitu wa Mabwepande.
Madaktari wakiwa wamepigwa butwaa nje ya viwanja vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia tukio hilo.
Wauguzi wakiwa nje ya wodi ya Kibasila wakitafakari jambo kufuatia jambo hilo
No comments:
Post a Comment