Serikali ya Ethiopia imelaumiwa
kwa kuwahamisha kwa nguvu maelfu ya watu kutoka mashamba yao ili kuacha
nafasi kwa upanzi wa miwa
Bonde hilo ambalo limeorodheshwa kama sehemu ya kuhifadhiwa duniani ,pia ndipo mahali bwawa kubwa limepangwa kujengwa. Ujenzi wa bwawa hilo tayari limezua utata.
Lakini serikali ya Ethiopia imekanusha madai hayo ya kuwahamisha watu kwa nguvu huku ikijitetea kwamba mradi huo utazalisha nafasi zaidi za kazi.
Nalo shirika la Human Rights Watch limesema kuwa maafisa wa usalama wanawahamisha watu kwa nguvu kutoka eneo hilo na kuwalazimisha kurudi katika ardhi zao za kiasili.
Katika ripoti yao, shirika hilo limesema wakati waliopkuwa wakizuru eneo hilo mwezi wa June 2011,walishuhudia makundi ya kijeshi yakiwahangaisha na kutisha watu ili wahame na kutoa nafasi kwa upanzi wa miwa. Katika harakati hizo wanajeshi wanadaiwa walikuwa wakiiba na kuwauwa mifugo.
Hata hivyo serikali ya Ethiopia imekanusha madai hayo.
Msemaji wa serikali Bwana Bereket Simon amesema palipokuwa na haja ya kuwahamisha watu , wahusika sote walishauriwa na pia kushirikishwa.
No comments:
Post a Comment