Mripuaji wa kujitoa mhanga amemuuwa kamanda wa jeshi kusini
mwa Yemen katika shambulio lililofanyika leo katika mji wa bandari
wa Aden.
Jenerali Salem Ali Qoton aliuawa karibu na nyumbani kwake katika eneo la Mansoura, na watu wengine wanne walijeruhiwa. Taarifa zinasema mshambuliaji alimkabidhi karatasi Jenerali huyo wakati akitembea kuelekea ofisini kwake, akapeana naye mkono na baadae kujiripua .
Jenerali huyo, aliyekuwa kamanda mkuu wa jeshi kusini mwa Yemen, aliongoza hujuma ya mwezi mmoja dhidi ya Al-Qaeda na kusababisha wapiganaji wa kundi hilo kuihama miji na vijiji kadhaa katika wilaya za Abyan na Shabwa, ambazo walizidhibiti kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Shambulio la leo asubuhi lilifanyika wakati Al-Qaeda wakiihama ngome yao ya mwisho katika mji wa Azzan.

No comments:
Post a Comment