Habari kubwa sasa hivi kwa
wadau wa muziki Morogoro ni kuhusu kifo cha msanii wa hiphop Mbudu
Square, rafiki wa karibu na aliefanya kazi kwa ukaribu na Afande Sele,
Bele 9 na wengine, alikua maarufu sana Morogoro kwa sababu ya kuitumia
vizuri nafasi aliyokua anapata kwenye show mbalimbali za Morogoro.
Mbudu amefariki jana kwa ajali
ya pikipiki Morogoro ambapo alikua kapakizwa, na chanzo cha ajali ni
gari lililokuja kwa nyumba na kuigonga pikipiki, Mbudu alifariki dunia
kwenye eneo la ajali kutokana na kupasuka kichwa.
Mpaka anafariki dunia, Mbudu alikua akiperform sana pamoja na Afande Sele katika showz mbalimbali Tanzania.
habari kwa hisani ya millardayo.com
No comments:
Post a Comment