MSHAMBULIAJI
wa timu ya Taifa ya Rwanda(Amavubi), Meddie Kagere amekiri kufanya
mazungumza na klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam na amefanya hivyo
kutokana na kuvutiwa na klabu hiyo ya Jangwani.Hata hivyo, hatma
ya mazungumzo hayo anatarajia kuyaanika hadharani baada ya pambano la
kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2012 kati ya
Rwanda na Benin mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza na Mwananchi
kwa simu toka Kigali, Rwanda, Kagere anayeichezea Polisi Rwanda, alisema
amepokea ofa kadhaa toka klabu za ndani na nje, lakini mpango wake wa
sasa ni kujiunga na Yanga.
"Niweke wazi kwamba, Yanga wananihitaji
na tayari nimefanya nao mazungumzo ya awali. Upo uwezekano nikajiunga
nao ingawa hatujaafikiana moja kwa moja kwani nimewaambia wasubiri.
"Siyo
Yanga tu, zipo klabu nyingi zinanihitaji ikiwemo Simba ya hapo Tanzania
lakini zaidi ningependelea kucheza Yanga kuliko Simba," alisema Kagere
na kuongeza kuwa:
"Huwa nazungumza na Haruna (Niyonzima) kuhusu
ligi ya Tanzania ndiye yeye ndiyo anayenishawishi kuja. Mimi na yeye
tunaelewana tunapocheza pamoja timu ya taifa na bila shaka ushirikiano
wetu na wachezaji wengine tunaweza kuipa Yanga mafanikio." |
|
No comments:
Post a Comment