Thursday, June 14, 2012

'Kauli ya wachezaji mashoga siyo yangu'

MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa Italia, Antonio Cassano ameomba radhi kufuatia kauli yake kwamba kwenye kikosi cha timu yao ya taifa hakuna wachezaji mashoga.Cassano (29) anayecheza timu ya AC Milan, alikariria akisema anaamini hakuna mchezaji shoga kwenye kikosi chao kinachoshiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya zinazoendelea nchini Poland na Ukraine.
Lakini baadaye alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema, maelezo yake yalikaririwa vibaya.
"Hakika najuta kwa sababu kauli yangu imetafsiriwa vibaya na kwenda kinyume na haki za wanaume mashoga," alisema.

"Sikuwa na maana ya kumsema wala kumlenga yeyote, sina mamlaka ya kuhoji uhuru wa watu katika suala la mapenzi.
"Nilichoongea ni kwamba, tatizo hilo haliko upande wangu na sina mamlaka ya kutoa hukumu kwa kile mtu anachotaka kukifanya."
Cassano aliulizwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kama anadhani kwenye kikosi chao kuna wachezaji mashoga."Kocha aliniambia kwamba mtaniuliza swali kama hili. Kama nikisema nachofikiria...nadhani hakuna," alisema.
 


No comments:

Post a Comment