Mahakama Kuu ya Pakistan yampa Waziri Mkuu mpya wiki mbili kumshitaki Rais
Mahakama Kuu ya Pakistan imempa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo, Raja Pervez Ashraf, muda wa wiki mbili kufungua kesi ya ufisadi dhidi ya Rais Asif Ali Zardari.
Ashraf aliapishwa wiki iliyopita baada ya mtangulizi wake, Yusuf Raza Gilani, kuenguliwa na mahakama hiyo kwa kudharau amri ya kuiomba Uswisi kuanzisha tena uchunguzi wa wizi wa fedha dhidi ya Rais Zardari.
Tayari Ashraf ameashiria kwamba hatoifungua tena kesi hiyo ya ufisadi.
Gilani na chama chake cha Pakistan People's Party, PPP, walikuwa wamejenga hoja kwamba rais anakuwa na kinga anapokuwa madarakani.
Mzozo baina ya mahakama na serikali unaweza kusababisha uchaguzi mpya.
Zardari anatuhumiwa kutokana na wizi wa mamilioni ya dola uliofanyika katika miaka ya 1990 wakati mke wake, Marehemu Benazir Bhutto, alipokuwa waziri mkuu wa Pakistan.
No comments:
Post a Comment