Idadi ya watu waliokufa katika mapigano yameliyozuka kutokana na mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye itikadi kali na askari nchini Nigeria imefikia watu 18.
Watu waliokuwa na silaha wamevamia kituo cha polisi na jela kwenye miji mitatu ya nchi hiyo jana jioni na kusababisha mapambano baina yao na vikosi vya usalama.
Mapambano makali zaidi yanatajwa kuwa kwenye mji wa Kano mji wa pili kwa ukubwa nchini humo ulioko kaskazini.
Hadi sasa hakuna kikundi chochote kilichotangaza kuhusika na mashambulizi hayo lakini inaaminika yamefanywa na kundi la wanamgambo wenye msimamo mkali la Boko Haram.
Kundi hilo limeshasababisha vifo vya zaidi ya watu 1000 hadi sasa tangu katikati ya mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment