Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu
Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, kwa vyombo vya habari jana ilieleza kwamba bei hiyo inajumuisha gharama za kuunganisha maji kwa mara ya kwanza, mkodishaji na mwendeshaji.
Alisema kwa wateja wanaotumia maji kwa kiwango cha mililita za ujazo 0 hadi 5 kwa mwezi, bei itatozwa kulingana na gharama za mwendeshaji ambacho ni Sh. 604 kwa mililita za ujazo kwa mwaka 2012/13 wakati mwaka ujao gharama itakuwa ni Sh. 403 kwa ujazo huo.
Kuhusu majitaka, alisema gharama hizo zimepanda kutoka Sh. 227 kwa mililita moja ya ujazo hadi Sh. 250 mwaka 2012/13 na Sh. 275 mwaka ujao kwa ujazo huo.
Alisema bei hizo zimeidhinishwa baada ya Ewura na vyomboi vyake kupitia maombi yaliyowasilishwa kwenye mamlaka hiyo na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasa), mwaka mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment