Tuesday, June 12, 2012

Makanisa mawili yashambuliwa Nigeria

Mashambulio dhidi ya makanisa mawili nchini Nigeria yameuwa watu kama wane.
Mji wa Jos, Nigeria
Shambulio kubwa lilifanywa katika mji wa Jos, katikati mwa Nigeria.
Wakuu wanasema watu watatu walikufa na zaidi ya 40 kujeruhiwa wakati mshambuliaji wa kujitolea mhanga, alipojiripua nje ya kanisa.


Kishindo cha mripuko huo kilibomoa sehemu ya jengo.
Shambulio la pili lilifanywa katika mji wa Biu, kaskazini-mashariki mwa nchi.

Polisi walisema wanaume kadha waliokuwa na silaha, walifyatua risasi wakati wa ibada ya asubuhi, na kumuuwa mwanamke mmoja.
Hakuna aliyekiri kuhusika na mashambulio hayo.

Katika miezi ya karibuni, wapiganaji wa Kiislamu wa kundi la Boko Haram wamefanya mashambulio kadha kwa bunduki na mabomu.


No comments:

Post a Comment