Tuesday, June 12, 2012

ICC na kesi ya watuhumiwa wawili wa Kenya


Kesi  katika mahakama  ya kimataifa ya uhalifu , inayowakabili watuhumiwa wawili wa ngazi ya juu nchini Kenya, akiwemo mgombea mmoja wa Urais katika uchaguzi  mkuu mwaka ujao, inaweza kusikilizwa mjini The Hague mwezi Machi  utakapoitishwa uchaguzi mkuu.

 Mahakama hiyo iliamua mwezi Januari mwaka huu kwamba  Waziri wa zamani William Ruto mwenye umri wa miaka 45 na mkuu wa kituo cha Redio Joshua Arap Sang mwenye umri wa miaka 36 washtakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binaadamu, kwa kuandaa mpango wa kuwashambulia wafuasi wa chama tawala, baada ya kuzuka mabishano juu ya matokeo ya uchaguzi, miaka mitano iliopita.


 Ruto anatajwa kuwa miongoni mwa wagombea  wakuu wa Urais katika uchaguzi mkuu ujao. Pande zote mbili-mashtaka na utetezi- zimekubaliana  kuanza kwa kesi hiyo kuwe Machi  2013.

Rais wa mahakama ya The Hague, Jaji Kuniko Ozaki amesema tarehe  rasmi iatatangazwa kabla ya mapumziko ya msimu wa joto kuanza Julai 14 .

No comments:

Post a Comment