Monday, June 11, 2012

Makanisa yashambuliwa Nigeria

Watu wasiopungua sita waliuwawa jana na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga alipojilipua nje ya kanisa moja nchini Nigeria na watu waliokuwa na bunduki kulishambulia kanisa lengine kaskazini mwa nchi hiyo.

 Mshambuliaji huyo aliliendesha gari lake hadi katika uwanja wa kanisa moja mjini Jos na kulipua bomu karibu na kanisa hilo. Polisi wamesema hakuna aliyeuwawa katika hujuma hiyo, lakini vijana waliwashambulia watu waliokuwepo kulipiza kisasi na kuwaua wawili.
 Katika shambulizi la ufyetuliaji risasi, mtu mmoja aliuwawa katika kanisa la mjini Biu katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria. Kundi la wanaitikadi kali la Boko Haram limedai kuhusika na mashambulizi hayo.

No comments:

Post a Comment