Monday, June 11, 2012

Watu takriban 35 wauwawa Syria

Watu wasiopungua 35 waliuwawa jana nchini Syria katika mashambulizi mabaya kuwahi kushuhudiwa tangu kusambaratika kwa makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya kusitisha mapigano mwezi Aprili mwaka huu.


 Mauaji hayo yalijiri wakati vikosi vya rais wa nchi hiyo, Bashar al Assad vilipokuwa vikiimarisha jitihada za kuudhibiti mkoa wa Homs.
 Kwa upande mwingine upinzani hapo jana ulimchagua kiongozi mpya kufuatia ukosoaji dhidi ya kiongozi aliyekuwepo kwamba alikuwa dikteta na kwamba kundi hilo lilikuwa likidhibitiwa na watu wenye misimamo mikali ya dini ya kiislamu.

No comments:

Post a Comment