WAGONJWA
katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, mjini Moshi wameanza kuonja shubiri
ya mgomo, baada ya madaktari zaidi ya 80 wa hospitali hiyo, kuanza rasmi
mgomo usiokuwa na kikomo.
Habari zinadai kuwa hatua ya madaktari
walioko kwenye majaribio na wale wanaosomea udaktari bingwa, inatokana
na vikao vyao vilivyofanyika jana asubuhi.
“Intern Doctors ndio
wameweka vifaa vyao chini na wameondoka wote na hawako wodini,hawa wako
kati ya 70 na 80 hivi hali sio nzuri hata kidogo,”alidokeza daktari
mmoja bingwa katika hospitali hiyo.
Hospitali ya KCMC ina aina
mbili za madaktari ambao ni wale walioajiriwa na Serikali na wale
walioajiriwa na Shirika la kidini la Msamaria Mwema (GSF) na waliogoma
ni wale wa Serikali.
Kwa mujibu wa daktari huyo, madaktari hao
tayari wameshamaliza mafunzo yao ya udaktari lakini kwa sasa wako,
katika majaribio kwa vitendo.Habari zilisema madaktari wanaosomea
ubingwa walikuwa katika maandalizi ya mwisho ya kuanza mgomo na baadhi
yao hawakuwa wakitoa huduma, jambo lilioashiria kuwapo kwa mgomo baridi.
Taarifa
zilizopatikana baadaye jana alasiri zilisema madaktari waliokuwa
wakitoa huduma ni wale mabingwa na kwamba haijulikani wengine walikuwa
wapi.Muuguzi mmoja katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi
maalumu, aliliambia gazeti hili kuwa huduma zilikuwa zinatolewa na
madaktari bingwa tu na wale ambao ajira zao ziko shirika la GSF, ambao
kwa Idadi ni wachache.
Mkazi mmoja wa Moshi, Raymond Mushi
alisema kaka yake ambaye anasumbuliwa na kuziba kwa kibofu cha mkojo,
alitakiwa kufanyiwa upasuaji jana, lakini kwa sababu ya mgomo
aliruhusiwa kurudi nyumbani.Mkurugenzi Mwendeshaji wa Hospitali
ya KCMC, Dk. Moshi Ntabaye, hakupatikana kuzungumzia habari hizi kwa
sababu simu yake, ilikuwa haipokelewi na ilielezwa kuwa alikuwa katika
vikao vya kunusuru mgomo.
Taarifa kutoka Hospitali ya Mkoa wa
Kilimanjaro ya Mawenzi na hospitali za Wilaya za Same,Mwanga na Hai
zilisema huduma za matababu zilikuwa zikiendelea kama kawaida.
Mkuu
wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alisema hakuwa na taarifa za kuanza
kwa mgomo kwa kuwa alikuwa bungeni mjini Dodoma na kuahidi kufuatilia
suala hilo kwa ukaribu.
Habari kutoka Mbeya zilisema wagonjwa
katika Hospitali ya Rufaa Mbeya na ile ya Kitengo cha Wazazi ya Meta,
jana waliendelea kusotea huduma kufuatia mgomo unaoendelea.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hiyi katika huko Meta, baadhi ya wajawazito
walisema wanaendelea kusotea matibabu kufuatia mgomo wa madaktari.
"Tumekaa
tu hapa tangu saa 1:00 asubuhi,hakuna mganga anayejali na manesi
waliopo hapa wanatushauri tuondoke tu,”alisema Mariam Christopher.
Muuguzi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alikiri kuwa hali ni mbaya na kwamba hiyo inatokana na mgomo wa madaktari.
Mganga
Mkuu wa Hospiatali ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina, alikiri kuwapokea
wanawake wengi wajawazito wakitokea Hospiatali ya wazazi ya Meta.
Alisema hata hivyo hospitali hiyo sasa imezidiwa na wagonjwa wanaotoka katika hospitali mbalimbali.
“Nikweli
tunapokea wagonjwa wengi ambao ni akina wajawazito wakitokea Meta,hali
sasa inaelekea kuwa mbaya sana hapa kwetu kwani miundombinu katika wodi
ya akina mama wajawazito haitoshi," alisema Dk Mhina.
Mkurugenzi
wa hospitali hiyo Dk Eliuter Samky hakupatikana kutokana na kile
kilichoezwa kuwa alikuwa na kikao cha dharura kilichoongozwa na Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.
Habari kutoka Mwanza zilisema hali katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando bado ni tete.
Akizungumza
na Mwananchi, mmoja wa madaktari waliogoma Dk Geogre Andrian alisema
hawapo tayari kurudi kazini hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai
yao.
“Huu ni wakati wa ukweli na uwazi kama Serikali imetekeleza
nusu ya madai yetu kwani nini hawajaelezea wazi yale ambayo wameyafanya
ili watanzania wote waweze kushuhudia utekelezwaji wa madai
hayo,”alihoji Dk Adriano.
Aliendelea kwa kusema kuwa madakrati
waliopo katika mgomo ni madkataria mabao ni wazalendo na kudai kuwe
wengi wa madaktari wemekimbilia nchi za nje kwa sababu huko wanapata
maslahi mazuri.
Akitolea mfano wa nchini Rwanda alisema kuwa
madaktari huko wanalipwa kiasi cha dola 15000 na kusema kuwa hiyo ni
moja ya nchi katika afrika masharikia mabayo inawajali madaktari wake.
Jijini Dar es Salaam, habari zilisema madaktari wanaofanya kazi katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili ni wakuu wa idara na vitengo. Mmoja wa maaofisa katika hospitali hiyo, alisema mgomo unaendelea, umeathiri utoaji wa huduma katika Hospitali ya Muhimbili.
“
Godfrey Kahango, Mbeya, Daniel Mjema,Moshi, Brandy Nelson, Mbeya, Geofrey Nyang’oro |
No comments:
Post a Comment