Wednesday, June 20, 2012

Raia 8 wauwawa Afghanistan

Raia wapatao wanane wameuwawa katika mkoa wa Helmand, kusini mwa Afghanistan wakati bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lilipolipuka.

 Watu wengine kadhaa wajeruhiwa katika hujuma hiyo. 


Wakati huo huo, mwanajeshi mmoja wa kigeni ameuwawa kwenye shambulizi lengine tofauti katika mkoa wa Kandahar. Kwa mujibu wa maafisa wa Afghanistan watu watatu waliokuwa wamejihami na bunduki na kuvalia sare za polisi, waliwafyetilia risasi wanajeshi wa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani Afghanistan, ISAF, na kumuua mwanajeshi huyo.

 Afisa wa NATO, Kanali Jimmie Cummings, amesema hili ni shambulizi la 17 la vikosi vya usalama vya Afghanistan au watu binafsi waliovalia sare za vikosi vya usalama vya Afghanistan dhidi ya majeshi yanayoongozwa na NATO katika mwaka huu, ambapo wanajeshi wasiopungua 23 wameuwawa.

No comments:

Post a Comment