Wednesday, June 20, 2012

Mahakama ya Pakistan yamtimua waziri mkuu

Mahakama ya juu nchini Pakistan imepitisha uamuzi kwamba waziri mkuu wa nchi hiyo, Yousuf Raza Gilani, hastahiki kuwa madarakani kutokana na kutiwa hatiani katika kesi ya kuibeza mahakama.

 Katika hukumu yake ya leo mahakama hiyo imeiamuru tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imfute kazi rasmi Gilani na kusema hakuwa waziri mkuu kwa njia iliyo halali tangu Aprili mwaka huu, wakati alipotiwa hatiani kwa kukataa kumfungulia kesi bosi wake, rais wa Pakistan, Asif Ali Zardari. Kesi hiyo ya miaka ya 1990 inazihusisha mahakama za nchini Uswisi.


 Hukumu hiyo inakamilisha mchakato ulioanza na uamuzi wa mahakama kuu mnamo mwaka 2009 ilipoiamuru serikali kuitaka Uswisi kuzifungua tena kesi dhidi ya rais Zardari. 

Gilani alikataa akisema rais alikuwa na kinga dhidi ya mashtaka akiwa madarakani, na mwezi Januari mwaka huu mahakama ikamfungulia kesi ya kuibeza.

No comments:

Post a Comment