Serikali
imesema madai ya madaktari ya kutaka kuongezewa maslahi yatatolewa
maamuzi kesho baada ya suala hilo kuwa kwenye majadiliano.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana
jijini Dar es Salaam kwa njia ya simu, Waziri wa Afya na Utawi wa Jamii,
Dk. Hussen Mwinyi, alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa suala hilo
kwa kuwa bado liko kwenye mazungumzo na kuahidi kulitolea taarifa kesho.
"Nikizungumzia kwa sasa nitakuwa
nimeingilia mazungumzo ambayo yanaendelea hivyo nipe muda kidogo mpaka
Jumatatu nitatoa taarifa dhidi ya suala hilo," alisema Dk. Mwinyi
Wiki iliyopita madaktari waliipa serikali
muda wa wiki mbili kuhakikisha inatimiza madai yao na kama itashindwa
kufanya hivyo wataandaa mgomo nchi nzima.
Pia madaktari hao wamepinga vikali
kuipokea ripoti ya kamati ya serikali ambayo ilipewa kazi ya
kushughulikia sakata la madaktari.
Walieleza kuwa taarifa ya kamati hiyo
imeshindwa kueleza jinsi gani itashughulikia madai yao ikiwemo suala la
nyongeza ya mshahara ambapo walitaka iwe sh milion 3.5 kwa kima cha
chini.
Hivyo kutokana na suala hilo, madaktari
waliipa serikali siku 14 kuhakikisha inatekeleza madai yao na endapo
isipofanya hivyo wanajianda kufanya mgomo kwa madaktari wote.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment