Monday, June 25, 2012

Shambulizi la guruneti laua watu kadhaa Mombasa

Mtu mmoja aliuwawa jana na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati guruneti lilipovurumishwa ndani ya baa moja katika kitongoji cha Mishomoroni katika mji wa bandari wa Mombasa katika pwani ya Kenya.

Hujuma hiyo dhidi ya baa la Jericho, ilifanywa wakati wateja na mashabiki wa soka walipokuwa wakitazama mchuano wa robo fainali ya mashindano ya kandanda ya kombe la mataifa ya Ulaya UEFA EURO 2012 kati ya Italia na England uliokuwa ukichezwa mjini Kiev nchini Ukraine.


 Kamanda wa jeshi la polisi mkoani pwani, Aggrey Adoli, amesema watu watatu kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mahututi. Shambulizi hilo lilifanywa siku mbili tu baada ya Marekani kuwaonya raia wake kuhusu uwezekano wa kufanyika shambulizi la kigaidi mjini Mombasa.

 Maafisa wa Kenya walilaani onyo hilo la Marekani lililotolewa Ijumaa iliyopita, wakisema lingewatatiza watalii na kwamba lilikuwa ni hujuma dhidi ya uchumi wake

No comments:

Post a Comment