Monday, June 25, 2012

Al Mahmoudi arudishwa Tunisia

Tunisia imemuwasilisha kwa viongozi wa Libya, Baghdadi al Mahmoudi, aliyekuwa waziri mkuu wa mwisho wa Libya chini ya utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo, Muammar Gadhafi.

Al Mahmoudi, ni kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kurejeshwa Libya kushtakiwa tangu Gadhafi alipoondolewa madarakani mwezi Agosti mwaka jana.


 Mawakili na wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu wameelezea wasiwasi wao kwamba al Mahmoudi huenda akanyongwa iwapo atarejea nchini Libya.

 Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP rais wa Tunisia, Moncef Marzouki jana alilaani hatua ya kumrejesha kiongozi huyo Libya akisema si halali.

Katika taarifa yake alisema waziri mkuu wa Tunisia aliidhinisha kurejeshwa al Mahmoudi, bila idhini yake. al Mahmoudi alikimbilia Tunisia mwezi Septemba mwaka jana ambako alitiwa mbaroni kwa kuingia bila kibali.

No comments:

Post a Comment