Monday, June 25, 2012

Waziri wa Ulinzi na mshauri wake wafukuzwa kazi Nigeria

Rais Goodluck Jonatahan wa Nigeria, amemfukuza kazi Waziri wa ulinzi pamoja na mshauri wake, hku kukiwana ongezeko jipya la mashambulizi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali la Boko Haramu. 

Taarifa za kufukuzwa kazi Waziri Bello Mohammed na mshauri wake Andrew Owoye Azazi zimetolewa na msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo Reuben Abati na kuchapishwa kwenye gazeti moja maarufu la kila siku nchini humo.


Nafasi ya Azazi imechukuliwa na Kanali mstaafu Sambo Dasuki kiongozi maarufu kutoka eneo la kaskazini na binamu wa Sultani wa himaya ya Sokoto.

Dasuki alihusishwa pia katika jaribio la kufanya mapinduzi mwaka 1995 dhidi ya utawala wa kidikteta wa Rais wa zamani San Abacha, na kukimbilia uhamishoni nchini Marekani. Hadi sasa hakuna taarifa kamili kuhusu mtu atakayechukua nafasi hiyo ya uwaziri wa ulinzi.

Uamuzi baada ya kurejea kutoka Rio

Rais Jonathan amechukua hatua hiyo mara baada ya kurejea kwenye mkutano wa mazingira duniani uliofanyika mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil. Uamuzi wa rais huyo kuhudhuria mkutano huo kimekosolewa vikali na watu mbalimbali nchini mwake, baada ya Boko Haramu kufanya mashambulizi kwenye makanisa Jumapili iliyopita mjini Kaduna.

 Kituo cha polisi Nigeria Kituo cha polisi Nigeria
Mashambulizi hayo yaliyozusha hasira miongoni mwa wakristo na kusababisha vurugu ambapo watu 110 waliuawa. Rais Jonathan aliondoka nchini humo siku ya Jumanne kwenda Brazil, licha ya kuwepo kwa mashambulizi hayo mapya.
Nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta, imegawika katika sehemu mbili ya kaskazini ambayo inakaliwa na waislamu na kusini inayokaliwa na wakristo.
Mshauri Azazi ni mshirika wa kisiasa wa Rais Jonathan amabye wanatokea sehemu moja jimbo la Balyesa lenye utajiri wa mafuta kusini mwa nchi hiyo. Azazi anashukuiwa na watu wa eneo la kaskazini kuhusika na machafuko hayo, kufuatia kauli yake aliyoitoa mwezi Aprili inayoonyesha kuwa matukio hayo yana msukumo wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment