Friday, June 22, 2012

Taliban washambulia hoteli mjini Kabul

Wapiganaji waliokuwa na makombora na silaha kali wamefanya shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya Hoteli katika eneo maarufu mjini Kabul huku kukiwa na taarifa kuwa wapiganaji hao wanawashikilia mateka watu kadha. Majeshi ya usalama ya Afghanistan pamoja na majeshi ya kimataifa wanajibu shambulio hilo katika katika mapambano yanayofanyika katika eneo la Ziwa Qargha nje kidogo ya mji mkuu wa Afghanistan.

Washambuliaji hao wanaonekana kuwalenga polisi na raia, jeshi la ISAF limesema na kuongeza kuwa kuna ripoti kwamba polisi na raia wameuwawa.
Kundi la Taliba limedai kuhusika na mashambulio hayo , muda mfupi baada ya rais Hamid Karzai kuonya kuwa mashambulio dhidi ya vituo mbali mbali bya polisi na wanajeshi yanazidi wakati majeshi hayo yakijitayarisha kuchukua jukumu la usalama wakati majeshi ya NATO yatakapoondoka mwaka 2014.

Naibu mkuu wa polisi mjini Kabul Daoud Amin amesema kuwa kwa mujibu wa walinzi wa hoteli, kulikuwa na washambuliaji watatu ndani ya hoteli hiyo, pamoja na raia kadha. Watu walioshuhudia wanaokimbia kutoka sehemu hiyo wamesema kuwa washambuliaji hao wanawashikilia mateka.

No comments:

Post a Comment