Thursday, June 28, 2012

Tume ya Katiba



kukusanya maoni yao kuhusu Katiba Mpya.

Taarifa ya tume hiyo kwa vyombo vya habari jana ilieleza kwamba mikoa hiyo ni Dodoma (Bahi), Kagera (Biharamulo), Kusini Pemba, Kusini Unguja (Kusini), Manyara (Mbulu), Pwani (Mafia), Shinyanga (Kahama) na Tanga (Lishoto). 


“Taratibu zote za kuanza kazi zimekamilika zikiwemo kuandaa ratiba na kuisambaza katika mikoa na wilaya husika. Wajumbe wa Tume na watumishi wa Sekretarieti wamejigawa katika makundi saba. Kila kundi litafanya mikutano katika mkoa mmoja isipokuwa kundi moja litakalofanya mikutano katika mikoa miwili ya Kusini Unguja na Kusini Pemba,” ilisema taarifa hiyo.

Tume imewaomba wananchi kuhudhuria mikutano hiyo na kutoa maoni yao kwa uwazi, uhuru na utulivu.

No comments:

Post a Comment