Saturday, June 30, 2012

Watu wanane wauawa kwa mabomu Irak

Mabomu matatu yaliotegwa katika pikipiki yaliripuka karibu na soko na kituo cha polisi na kuua watu wanane nchini  Irak Watu wengine kadhaa  walijeruhiwa .
Kwa mujibu wa maafisa  mripuko  huo uliyotokea katika mji wa Balad, kiasi ya kilometa 80 kaskazini mwa Baghadad, ni  mkasa mkubwa  kuwahi  kutokea katika miezi ya hivi karibuni tokea kuondoka kikosi cha mwisho cha Marekani Desemba mwaka jana.

Balad ni mji hasa wa Washia katika jimbo lenye Wasunni wengi la Salahuddin.
Kiasi ya watu 220 waliuwawa katika kipindi cha mwezi huu wa Juni ikiwa ni ongezeko kubwa la vitendo vya umwagikaji damu ambapo maafisa na wachambuzi wanahofia kwamba huenda ikawa ni sehemu ya jitihada za wapinzani  za kuanzisha tena machafuko kwa misingi ya kikabila. ..

No comments:

Post a Comment