Saturday, June 30, 2012

Kabila aahidi kulinda mipaka ya DRC

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo  amewalaumu waasi na wapiganaji kutoka nje ya taifa lake kwa kuendeleza machafuko katika maeneo ya mashariki mwa Kongo.
 Hata hivyo Rwanda imekwisha kanusha madai kwamba inalisaida jeshi lililoasi la waasi wa zamani wenye asili ya Kitutsi ambao kwa hivi sasa wanajulikana kama M23 ambao waliijuinga na jeshi na baadae kuasi.


 Akizungumza katika televisheni ya serikali , rais Kabila alisema sherehe za uhuru wa JKK, zitakugubikwa na vitendo vya uasi vinavyofanywa na wapiganaji wa waasi pamoja na wapiganaji kutoka nje ya taifa hilo.

Amesema vitendo hivyo vimeleta machafuko katika eneo la Kivu ya Kaskazini na kusababisha maelfu ya raia kuteseka na kutokuwa na usalama.
Kutoka na hali hiyo rais Kabila amesema kuimarisha usalama katika eneo hilo ni suala la kipaumbele, na kwa namna yeyote, kwa gharama yeyote watalilinda taifa na kulifanya kuwa nchi ya amani.             

No comments:

Post a Comment