Saturday, June 30, 2012

Baraza la Usalama laamua kuhusu Kony

Baraza  la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha vikosi vya Umoja wa Afrika kumkamata mbambe wa kivita Joseph Kony na kuliteketeza kundi lake la Lord's Resistance Army.
Nchi 15 wanachama wa baraza hilo zimeidhinisha jitahda zao za kikanda kukabiliana na kitisho na athari za shughuli za LRA.
Mpango huo unajumuisha kuongozwa wanajeshi 5,000 wa Umoja wa Afrika na jitihada za misaada ya kiutu.

 Mwaka 1990 waasi wa LRA walifanya mauwaji mabaya zaidi huko kaskazini mwa Uganda, lakini 2004 kwa kiasi kikubwa waliondolewa katika eneo hilo.
 Hata hivyo bado wanaendelea kuwashambulia  raia wa Uganda na nchi jirani tatu.
 Kundi hilo lina sifa mbaya ya kufanya mauaji ya kinyama, kuwakata viungo watu na kuwatumikisha watoto jeshini.           

No comments:

Post a Comment