Saturday, June 30, 2012

Mkutano wa mawaziri wa mataifa makubwa kuhusu Syria

Mkutano wa mawaziri wa mataifa yenye nguvu duniani ambao una lengo la kuokoa mpango wa amani Kofi Annan unatarajiwa kufanyika leo nchini Uswis.
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wa katibu  mkuu huyo wa  zamani  wa Umoja wa Mataifa.
 Mpango wa Annan unatoa wito wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itasimamia rasimu ya katiba mpya na uchaguzi.

 Moja kati ya maeneo muhimu ni kwamba serikali ya umoja wa kitaifa itajumuisha maafisa wa Assad na upinzani, lakini  haitawaashirikisha wale mabao kuwepo kwao kunaweza kuhujumu  jitihada za mpito na kuhatarisha utulivu na mchakato wa maridhiano.
 Wanadiplomasia wanasema hiyo ina maanisha Assad ataondolewa katika serikali lakini kinadharia hajaondolewa kushiriki kwake.
Duru za kidiplomasia zinasema  Urusi imelipinga pendekezo  hilo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton na mwenzake wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov wanatarajaiwa kukutana mjini St. Petersburg katika´jitihada ya kuondosha tafauti zao kuhusu mpango huo wa mpito.  

No comments:

Post a Comment