Saturday, June 30, 2012

Rais mteule wa Misri kuapishwa

Rais mteule wa Misri anaetarajiwa kuapishwa leo hii Mohammed Mursi, amesema hakuana mtu yeyote mwenye uwezo wa kuchukua mammlaka yake.
 Kiongozi huyo kutoka chama cha Udugu wa Kiislamu ameyasema hayo  huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wafuasi wa chama hicho waliokusanyika katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo.

 Mursi ameahidi kupinga njama zozote za kuondosha nguvu ya umma. Baraza tawala la kijeshi nchini humo limeahidi kukabidhi madaraka kwa rais mteule hapo kesho.
Lakini  Bataza hilo  pia  limejipa madaraka ambayo yanapunguza mamlaka ya rais.
Hatua ya kuvunjwa kwa bunge  hapo awali kumemlazimisha Mursi kula kiapo chake mbele ya Mahakama ya Katiba, ambayo ilitoa uamuzi dhidi ya bunge na ambalo mahakimu wake waliteuliwa na Mubarak.

No comments:

Post a Comment