Saturday, June 23, 2012

Waziri wa ulinzi na mshauri wake watimuliwa Nigeria

Rais Goodluck Jonatahan wa Nigeria, amemfukuza kazi Waziri wa ulinzi pamoja na mshauri wake, kitendo kinachofanyika wakati kukiwa na ongezeko jipya la mashambulizi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali la Boko Haramu.

Taarifa za kufukuzwa kazi Waziri Oluseyi Peteri na mshauri wake Andrew Owoye Azazi zimetolewa na msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo na kuchapishwa kwenye gazeti moja maarufu la kila siku nchini humo. Nafasi ya Azazi imechukuliwa na Kanali mstaafu Sambo Dasuki.


 Rais Jonathan amechukua hatua hiyo mara baada ya kurejea kwenye mkutano wa mazingira duniani uliofanyika mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil. Kitendo cha rais huyo kuhudhuria mkutano huo kimekosolewa vikali na watu mbalimbali nchini mwake, baada ya Boko Haramu kufanya mashambulizi kwenye makanisa Jumapili iliyopita mjini Kaduna na kuwauwa watu 110.

No comments:

Post a Comment