Omar Suleiman,
mtu aliyekuwa mkuu wa shirika la ujasusi nchini Misri chini ya utawala
wa rais aliyeondolewa mamlakani Hosni Mubarak, amefariki akiwa nchini
Marekani.
Generali Suleiman alifariki hospitalini mapema leo kwa mujibu wa taarifa za shirika la habari la Mena.Msaidizi wa generali huyo alisema kuwa kifo chake kimetokea ghafla wakati alipokuwa anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Hayati Suleiman aliteuliwa kama makamu wa rais kuhudumu katika siku za mwisho za utawala wa Mubarak.
Hata hivyo alikuwa na nia ya kugombea urais mwaka huu lakini akaondolewa nje ya shughuli hiyo kwa sababu zisizojulikana.
"alikuwa sawa tu. Lakini ghafla ikatokea tu alipokuwa anapokea matibabu mjini Cleveland," alisema msaidizi wake, Hussein Kamal.
Bwana Kamal alisema kuwa maandalizi yanafanywa ili kuleta mwili wake nchini Msiri kwa maziko.
Alikuwa makamu wa kwanza wa rais nchini Misri baada ya miaka 30 huku uteuzi wake ukifanywa tarehe 29 mwezi Januari mwaka 2011,siku nne baada ya harakati za mapinduzi kuanza dhidi ya uliokuwa utawala wa Mubarak.
Wiki mbili baadaye, alionekana katika runinga ya taifa akitoa tangazo la kujiuzulu kwa Mubarak na hivyo kusababisha watu kusherehekea katika midani ya Tahrir ambalo lilikuwa kitovu cha mapinduzi ya Mubaraka.
Baada ya kukosa kupata saini za kutosha kuweza kusimama kama kiongozi wa kwanza aliyekuwa katika uwala wa Mubarak mwaka huu, Suleiman aliondoka nchini humo ikisemekana alikuwa anaenda Abu Dhabi.
Mwandishi wa BBC Jon Leyne mjini Cairo anasema kuwa Omar Suleiman alikuwa mtu muhimu katika utawala wa Mubarak.
Kama mkuu wa ujasusi, Suleiman alisaidia kudhibiti idara ya polisi ambayo ilisaidia sana kutoa ulinzi kwa Mubarak alipokuwa mamlakani.
Lakini rais pia alimtegemea sana kama jasusi akisimamia maswala magumu kati ya nchi hiyo na waisraeli, wapalestina na wamarekani.
No comments:
Post a Comment