Wednesday, July 4, 2012

Marekani yaongeza majeshi Ghuba

Gazeti la Washington Post la Marekani limeripoti kuwa nchi hiyo imeongeza vikosi vyake katika nchin za Ghuba katika miezi ya hivi karibuni. 
Lengo la ongezeko hilo, linasema ni kuizuia Iran kuuziba mlango wa bahari wa Hormuz, ambao ni muhimu kwa usafirishaji wa mafuta kuelekea nchi za Magharibi. 
Msuguano baina ya Marekani na Irani umezidi kuongezeka kutokana na mpango wa Iran wa nyuklia, ambao Marekani na mataifa mengine ya Magharibi yanadai unalenga kutengeneza bomu la atomik. 

Iko hofu kuwa wanajeshi hao wa Marekani wanajianda kuvishambulia vituo vya Iran vya nyuklia. Jana vikosi maalum vya  jeshi la mapinduzi la Iran vilianza mazoezi ya kivita kwa siku tatu ambapo yanalenga mifano ya vituo vya nchi za Magharibi.
 Kamanda wa kikosi maalum cha jeshi la mapinduzi, Jenerali Hosseim Salami, alisema Iran inafanya majaribio ya makombora ya masafa marefu na ya kati, katika kuitikia vitisho kutoka kwa Marekani na Israel vya kutaka  kuishambulia nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment