Wednesday, July 4, 2012

Wairan walipanga kufanya mashambulizi Kenya

Wairani wawili waliowaongoza maafisa wa usalama mahala ambapo shehena ya vifaa vya kuripuka ilikuwa imefichwa walipanga kuvishambulia vituo vya Israel, Marekani, Uingereza na Saudi Arabia nchini Kenya. 

Hayo yalisemwa jana na maafisa wa Kenya wakati walipozungumza na shirika la habari la Associated Press. 
Afisa mmoja amesema Wairani hao ambao walikamatwa tarehe 19 mwezi uliopita, wanaaminiwa kuwa ni wanachama wa kikosi maalumu cha jeshi la mapinduzi la Iran kinachokabiliana na masilahi ya kigeni. 

  Washukiwa hao, Ahmad Abolfathi Mohammad na Sayed Mansour Mousavi, walifikishwa mbele ya mahakama moja ya Kenya Juni 25, ambapo Mohammed alisema alihojiwa na maafisa wa usalama wa Israel. 


Ubalozi wa Israel nchini Kenya haukusema lolote kuhusu madai hayo. Wakati huo huo, Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, jana aliishutumu Iran kwa kupanga mashambulizi dhidi ya Israel nchini Kenya kufuatia kukamatwa kwa Wairani hao wawili.

No comments:

Post a Comment