Maafisa nchini Kenya wanasema raia wawili wa Iran waliokamatwa nchini humo hivi karibuni na kugunduliwa kasha la mripuko, walipanga kuyashambulia maeneo yenye maslahi ya Marekani, Uingereza , Israel na Saudi Arabia.
Shambulizi la bomu katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998
Wakati hayo yakifichuliwa , kumekuweko na tetesi kwamba hujuma zao zinahusiana na kile kinachoendelea nchini Somalia. Mohamed Abdulrahman amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Ahmed Rajab, aliyoko mjini Nairobi na kwanza alimuuliza kama kuna uwezekano wa matukio hayo kuwa na uhusiano na vita vinavyoendeshwa na waasi wa Al-Shabaab nchini Somalia.
No comments:
Post a Comment