Tuesday, July 17, 2012

Mkutano wa Umoja wa Afrika kumalizika leo.

Mkutano wa viongozi wakuu wa Umoja wa Afrika unamalizika leo mjini Addis Ababa Ethiopia baada ya kumchagua Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini Zuma kuwa Kiongozi wa kwanza mwanamke wa Halmashauri Kuu ya Umoja huo.
Vyombo vya habari nchini Afrika ya Kusini vimeupongeza uteuzi huo na kusema kuwa ni ushindi mkubwa kisisa kwa nchi hiyo, Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC  na bara zima.
Viongozi na raia nchini humo wana matumaini kuwa mwanasiasa huyo ataimarisha mahusiano baina ya mataifa ya Afrika
. Uteuzi huo umemaliza kinyang'anyiro cha uongozi cha muda mrefu juu ya nani anafaa kuwa kiongozi wa umoja huo.

Anakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza umoja huo, na anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuimarisha amani barani humo katikati ya mzozo wa kisiasa kwenye nchi kama Mali, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pamoja na mvutano baina ya Sudan na Sudan Kusini. Mkutano wa umoja huo mwezi Januari mwaka huu, haukuweza mshindi baada ya  Bibi Zuma na mpinzani wake aliyekuwa akishikilia wadhifa huo Jean Ping  kutoka  Gabon kushindwa kupata theluthi mbili  zinazohitajika.     

No comments:

Post a Comment