Tuesday, July 17, 2012

Mubarak aamriwa kurudi gerezani

Mwendesha mashitaka mkuu wa Misri leo ameamuru kurejeshwa gerezani Rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak baada ya kulazwa hospitalini mjini Cairo kwa takribani kipindi cha mwezi mmoja mjini  kutokana na matatizo ya kiafya.

Mwendesha mashitaka huyo Abdel Meguid Mahmud ametoa amri ya kusafirishwa Mubarak kutoka hospitali ya kijeshi ya Maadi kurudi kwenye hospitali ya gereza la Tora baada ya kuimarika kwa afya yake.

 Tarehe 4 mwezi Julai mwaka huu, Mahmud alitoa amri ya kuundwa kwa jopo la madaktari ili kuchunguza afya ya Mubarak mwenye umri wa miaka 84  kuona  kama anaweza kurejeshwa tena gerezani.

 Madaktari hao walikubaliana kuwa afya ya kiongozi huyo  kutokana na matibabu  aliyopewa ni nzuri kwa mtu mwenye umri kama huo.
Jopo hilo halikuona haja ya Mubarak kuendelea kubakia kwenye hospitali ya jeshi  au nyengine.

No comments:

Post a Comment