Tuesday, July 17, 2012

Viongozi wa Somalia na ufisadi

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa viongozi wanaohusika na vitendo vya rushwa nchini Somalia ni lazima wakabiliane na vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bila kuchelewa ikisisitiza kuwa asilimia 70 ya mapato ya taifa hilo yaliibwa au kufanyiwa matumizi mabaya.
Ripoti hiyo ambayo inasema viongozi muhimu wa ngazi za juu serikalini akiwemo Rais  Sharif Sheikh Ahmed na spika wa bunge Sharif Hasasan  wamehusika na rushwa na hivyo kuimarisha malengo ya kundi la wanamgambo wa kiislamu wa itakadi kali la al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa al-Qaeda.

Ripoti hiyo inatoa wito kwa baraza la usalama kuweka vikwazo hivyo bila kuchelewa.
 Serikali ya mpito ya Shirikisho la Somalia inayofadhiliwa na mataifa ya magharibi, inamaliza muda wake mwezi ujao huku baadhi ya viongozi wakiwa na matumaini ya kuendelea kubakia madarakani hapo baadae.


Wengi wa viongozi hao wanashutumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa. Ripoti hiyo imeandaliwa na kundi la waangalizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia na Eritrea.

No comments:

Post a Comment