Tuesday, July 17, 2012

Mashujaa wa Kenya mahakamani London


Gereza la Mau Mau

Ombi la raia wanne mashujaa wa uhuru wa Kenya kutaka kukubaliwa kufungua kesi dhidi ya wakoloni wa Uingereza limeanza kusikilizwa katika mahakama kuu ya Uingereza London.
  Wanne hao ni pamoja na Paulo Nzilu, Wambugu wa Nyingi, Jane Muthoni Mara na jamii ya Susan Ngondi.
Mashujaa hao wa uhuru wa Kenya wanasema serikali ya Uingereza sharti ikiri kwamba maafisa wake walitekeleza dhuluma za kibinadamu katika iliyokua Koloni yake ya Kenya Afrika Mashariki.
 Wamesema kwamba serikali ya ukoloni katika miaka ya hamsini ilitangaza sheria ya hatari ambapo pia Vuguvugu la mau mau lilitangazwa kua la kigaidi na raia walioshukiwa kuwa wanachama walipelekwa katika vizuizi.
Wanavijiji Wengi kutoka jamii za Gikuyu, Embu, Meru na Kamba walikamatwa na maafisa wa kikoloni kwa kushukiwa kuunga au kuua wanachama wa Mau Mau na kuwekwa kizuizini ambapo walipitia dhuluma zikiwemo wanaume kuhakisa, ubakaji wa wanawake na mateso mengine.


Chini ya sheria za Uingereza, mtu hawezi kuwasilisha kesi katika mahakama zake inayohusisha matukio yaliyofanyika zaidi ya miaka sita. Hata hivyo mahakama inaweza kuridhia kesi iliyopita miaka sita kusikilizwa kulingana na uzito na matukio ya kesi hiyo.

Mashujaa wa Mau mau wamesisitiza kwamba dhuluma walizopitia ziangaziwe chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu ambayo ilichunguza kesi katika mauaji ya Ki- Nazi pamoja na uhalifu wa kivita kufuatia vita vya uliyokua muungano wa Kosovieti.

Baada ya hoja hizi Mahakama kuu ya Uingereza itaamua ikiwa wazee hawa wanaweza kufungua kesi dhidi ya serikali ya Uingereza kufuatia dhuluma wakati wa harakati za Uhuru.

No comments:

Post a Comment