Sunday, July 1, 2012

Mpango wa Annan kuhusu Syria wakubaliwa

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa  na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syria Kofi Annan amesema viongozi wa mataifa makubwa duniani kwa pamoja wameukubali mpango wake wa kipindi cha mpito nchini Syria. 

 Mpango huo unaelekeza  katika kuundwa  serikali ya mpito ikiwa na majukumu ya kusimamisha machafuko na kumaliza mvutano katika taifa hilo lililogubikwa na vita. 

Akizungumza na waandishi habari, Annan amesema mpango huo mpya unalenga kufikisha kikomo vurugu na ukiukwaji wa haki za binadamu. 

Hata hivyo Annan  hakuzungumza lolote lililofafanua moja kwa moja  kuhusu  majukumu ya rais wa sasa Bashar al-Assad katika serikali ya mpito itakayoundwa. 


Lakini amesema  hategemei raia wa Syria kuchagua watu walio na damu mikononi mwao.

No comments:

Post a Comment