Sunday, July 1, 2012

Wazu 47 wauwawa nchini Libya

Mapigano ya kikabila  kusini mwa Libya katika mji wa Kufra yanadaiwa kusababisha vifo vya takribani watu 47 na kuwaacha wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika kipindi cha siku tatu zilizopita

 Kwa mujibu wa Daktari pamoja na kiongozi wa kijamii waliozungumza na Shirikia la Habari la Ufaransa AFP, wamesema kiasi ya watu 32 wameuwawa katika maeneo mawili ya raia wa kabila la Toubou.

 Ijumaa iliyopita wapiganaji wa kabila la Toubou walivamia kambi ya jeshi la Libya, jeshi la ulinzi wa amani na kumuua mwanajeshi mmoja.

 Mji huo wenye  machafuko wa Kufra upo umbali wa kilometa 40,000, ukikutanisha mipaka ya mataifa ya Misri, Chad na Sudan.

No comments:

Post a Comment