Sunday, July 1, 2012

Ujerumani yakubali mpango wa kubana matumizi

Sera mbili muhimu barani Ulaya bado zinaning'inia nchini Ujerumani,  siku moja  baada ya mabunge yote mawili ya taifa hilo kuzipitisha. 

Chama cha mrengo mkali wa shoto (die linke) kimewasilisha rufaa yake katika Mahakama ya Katiba kikisema mfuko wa kusaidia kuleta uimara barani Ulaya ESM hauendi sawa na sheria za Ujerumani. 

 Uamuzi  kuhusu  rufaa  hiyo unaweza kuchukua wiki kadhaa. ESM ni mfuko wa uokozi katika kanda ya euro na umeundwa kinadharia kuwa na thamani  ya  euro  bilioni 500 ambazo mataifa  wanachama yanaweza  kukopa .


 Hapo Ijumaa bunge la Ujerumani vilevile limeidhinisha mpango wa udhibiti  wa bajeti  za  mataifa  ya  Umoja wa Ulaya. Katika mpango huo nchi zitakuwa zinakopa  katika vigezo maalum, au kukabiliwa na vikwazo kutoka  umoja  huo zitakapokwenda kinyume.

No comments:

Post a Comment