Sunday, July 1, 2012

Mji wa Timbuktu huko Mali waangamizwa

Kundi lenye mafungamano na mtandao wa al-Qaeda nchini Mali, limeanza kuharibu maeneo matakatifu ya Kiislamu katika mji wa Timbuktu baada ya UNESCO kuyataja maeneo hayo kuwa ni turathi za  dunia. 

Timbuktu, inajulikana kama "Mji wa watakatifu 333," ni eneo lenye misikiti mitatu ya kihistoria pamoja na makaburi kadhaa yaliyotambuliwa na UNESCO, kama shirika kubwa la uangalizi wa hazina ya utamaduni duniani.


 Shirika hilo tayari limekwisha sema hatua hiyo inaonekana dhahiri inatokana na hatua yao ya kuongeza eneo hilo katika rekodi zake za maeneo yake ya hifadhi. 

Nchi jirani na Mali katika maeneo ya Afrika magharibi zimekuwa na mkutano wa kujadili hali hiyo na wameomba Umoja wa Mataifa kusaidia kuingilia kijeshi ili kurejesha utulivu

No comments:

Post a Comment