Wiki moja kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi mkuu nchini Libya, kundi la wapiganaji wa waasi na
waandamanaji wamevamia na kuharibu mali katika ofisi ya tume ya uchaguzi
mjini benghazi.
Kwa mujibu wa mfumo mpya wa uchaguzi, eneo la magharibi na mji mkuu, litakuwa na jumla ya wabunge mia moja na mbili kati ya wangune mia mbili, huku eneo la mashariki likipewa viti sitini pekee.
Idadi iliyosalia imehifadhiwa kwa raia wa eneo la kusini.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli anasema kuna wasi wasi miongoni mwa raia mjini benghazi kuwa wao watatengwa na serikali kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa kanali gadaffi ambaye alipiga marufu vyama vyote vya kisiasa.
No comments:
Post a Comment