Tuesday, July 3, 2012

Chama cha zamani charudi madarakani Mexico

Chama tawala cha zamani nchini Mexico kimepata ushindi finyu katika uchaguzi mkuu uliyofanyika siku ya Jumapili baada ya kuwa nje ya serikali kwa muda wa miaka 12.
Mgombea wa chama hicho cha Institutional Revolutionary party (PRI), Enrique Pena Nieto, amejitangazia ushindi baada ya kukusanya asilimia 37.6 ya kura zilizopigwa.
Lakini mpinzani wake , Andres Maneul Lopez Obrador amakataa kukubali matokeo hadi kura ya miwsho itangazwe.
 Akiahidi kuchochea ukuaji wa uchumi na kupambana na dawa za kulevya, Nieto, mwenye umri wa miaka 45. anatarajiwa kuanza kazi mwezi Desemba baada ya kumalizika kwa kipindi cha miaka sita cha rais wa sasa. Akizungumzia ushindi wake huo, Nieto alisema: O-Ton (Nieta) Watu wa mexico wametupa nafasi nyingine, tutaonyesha shukrani zetu kwa kuwajibika.

 Hata hivyo, ushindi huo ni tofauti na ilivyotarajiwa hapo awali, ambapo kura za maoni zilikuwa zinampa Nieto tofauti ya kati ya silimia 10 na 15 mbele ya Obrador.

No comments:

Post a Comment