Tuesday, July 3, 2012

Waliotekwa nyara waokolewa Somalia

Wanajeshi wa Somalia na wa Kenya  wamewaokoa wafanya kazi wane  wa kigeni wenye kutoa misaada na ambao walikamatwa mahabusu ndani ya Somalia siku tatu baada baada ya kutekwa nyara katika nchi jirani ya Kenya.
 Hayo yamesemwa leo majeshi ya nchi hizo mbili. Wakionekana wamechoka, watu hao wanne walisafirishwa kwa ndege hadi Nairobi, ambako walikumbatiwa na wafanya kazi wenziwao baada ya kutoka kwenye helikopta ya jeshi.
 Shambulio hilo la ijumaa iliopita katika kambi ya wakimbizi ya Daddab, lilikuwa utekaji nyara wa mwanzo huko Kenya, tangu nchi hiyo ilipopeleka wanajeshi wake Somalia mwezi Oktoba mwaka jana, kukiangamiza kikundi cha wanamgambo wa al-Shabbab, chenye maingiliano na mtandao wa al-Qaeda. Dereva wa Kenya alipigwa risasi na kufa wakati wa utekaji nyara huo.

 Mmoja wa waliotekwa nyara, Qurat-Ul-ain Sadazai, raia wa Canada mwenye asili ya Pakistan, alisema wako na furaha kwamba wako hai na mkasa huo umekwisha. Watu hao wanalitumikia baraza la wakimbizi kutoka Norway.

No comments:

Post a Comment