Serikali ya Scotland imetangaza kwamba itaruhusu ndoa za watu wa jinsia moja.
Naibu waziri mkuu wa Scotland Bi Nicola Sturgeon amesema hatua hiyo ni ya maana sana na inastahili hasa kwa vile serikali yake inayoheshimu usawa wa kijinsia
Huenda Scotland ikajitokeza kuwa sehemu ya kwanza ya Uingereza kukubali ndoa za watu wa jinsia moja baada ya serikali ya SNP kutangaza mipango ya mabadiliko hayo.
Mawaziri wamesema kua muswada huo utajadiliwa mapema ikiashiria kua sherehe za kwanza huenda zikafanyika mwanzoni mwa mwaka 2015.
Viongozi wa kisiasa, mashirika yanayowania usawa na makundi ya imani yamefurahia hatua hio.
Hata hivyo ndoa ya jinsia moja inapingwa vikali na kanisa katoliki pamoja na Kanisa la Scotland.
Tangazo hilo lilifanywa kufuatia mashauriano ya serikali yaliyopokea majibu kutoka kwa watu 77,508.
Sheria ya Scotaland kwa Wapendanao wa wanaoishi pamoja wanaweza kuingia wenzi lakini serikali imesisitiza kua hapana taasisi yoyote ya kidini inayolazimishwa kuendesha sherehe za kufunga ndoa.
Serikali ya Scotland imesema kua itashirikiana na Mawaziri wengine Uingereza kuona kubadili sheria zinazowalinda watu mashuhuri wasichukuliwe hatua endapo watakataa kukemea au kukashifu ndoa za watu wa jinsia moja.
Waziri kiongozi wa Scotland, Nicola Sturgeon, alisema kua bado tuna amini Scotland iliyo na usawa na ndio sababu tunaendelea na mipango ya kuendesha ndoa za watu wa jinsia moja -tuna amini uwamuzi huu ndiyo jambo sawa.
No comments:
Post a Comment