Tuesday, July 24, 2012

Tunaposema ukaguzi wa vyombo vya usafiri tuna maana gani

Serikali imekuwa mstari wa mbele kufanya ukaguzi pindi ajali inapotokea na wakati mwingine hata kutumia kodi za wananchi ili kuunda tume ya kuchunguza ajali

Swali ni je walikuwa wapi kufanya ukaguzi kabla ya kutokea kwa ajali wahenga walisema kinga ni bora kuliko tiba juzi katika pita pita yangu nilipanda dala dala ndani yajiji la dar es salaam linaloekea maeno ya Masaki lakini nilishindwa kuvumilia na kuamua kupiga picha hii na ujiuliza je gari hili lilipotengenezwa na engineer aliweka jiwe hili
mbele kulia ni dereva akiwa hana wasi wasi kabisa tayari kwa kuanza safari kutoka ubungo terminal kuelekea Msasani huku karibu na Gea lever akiwa na jiwe ambalo kwa haraka sikujua kazi yake kwa haraka haraka unaweza sema gari hili haliwezi kuwa barabarabani lakini ukweli ni kwamba gari hili linafanya kazi na  mwenye gari anapokea hesabu jioni kama kawaida

swali langu je kutokana na uhaba au shida ya usafiri ndio sababu ya kuuza roho za watanzania kwa kuruhusu vyombo vibovu au tunasubiri ajali ili tuunde tume ya uchunguzi  watanzania wenzangu  kila mchuma janga hula na wakwao na sisi tunaokubali kupanda vyombo vibovu vya usafiri kwa kisingizio cha  ukosefu wa vyombo hivyo hebu tubadilike

kumbuka unapopata na majanga wakwanza kuadhirika ni wewe mwenyewe pamoja na familia yako haraka haraka haina baraka lakini kumbuka chelewa chelewa utakuta mwana si wako.

No comments:

Post a Comment