Maandamano baada ya uchaguzi nchini Kenya
Wanamziki watatu mashuhuri
nchini Kenya wameshtakiwa kwa kuchochoea chuki za kikabila kupitia
nyimbo zao. Wanamziki hao wanaoimba kwa lugha ya Kikuyu wametoa vibao
kumsifia Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta.
Mashtaka hayo yamewasilishwa mahakamani na Tume
ya uwiano na Maadili nchini Kenya {NCIC} ambayo iliundwa mwaka wa 2008
kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu.Bw Kinyatta amepinga kuunga
mkono wanamziki hao katika kutunga nyimbo za kumsifia.
Watatu hao ni pamoja na Kamande wa
Kioi, John De- Mathew, na Muigai Njoroge ambaye ni mwanamziki wa nyimbo
za dini na wamekanusha kuchochea chuki za kikabila mbele ya mahakama ya
Nairobi.Uhuru Kenyatta ni mwanawe Mwanzilishi wa taifa
la Kenya Jomo Kenyatta na anakabiliwa na kesi mbele ya Mahakama ya
Kimataifa ya Jinai-ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi.
Yeye pamoja na Wakenya wengine watatu
wamekanusha kuhusika na ghasia hizo ambapo zaidi ya watu 1,300 waliuawa
na wengine laki tatu kuachwa bila makao,Wanamziki hao wameachiwa kwa dhamana.Ikiwa watapatikana na hatia huenda wakafungwa jela miaka mitatu au faini ya dola 12,000.
No comments:
Post a Comment