Mjane wa kiongozi wa zamani wa Palestina, ameeleza kuwa
mume wake alikufa kutokana madini ya polonium yaliyo na sumu. Bi Suha
ataomba mwili wa marehemu mume wake ufukuliwe ili uweze kufanyiwa
uchunguzi zaidi.
Msemaji wa kituo hicho, Darcy Christen, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa wameshangazwa na kiasi cha madini ya polonium yaliyokutwa katika vitu vya Arafat.
Hata hivyo, Christen amesisitiza kuwa hawezi kusema kwa hakika kama Arafat aliuwawa kwa kupewa sumu au la, kwani dalili za ugonjwa zilizoandikwa katika ripoti ya daktari haziendani na dalili anazokuwa nazo mtu pale anapopewa sumu ya polonium.
Kituo cha televisheni cha Al-Jazeera, kimeeleza kwamba kituo cha utafiti cha Uswisi kilitumiwa nguo, mswaki pamoja na kilemba cha Arafat na mke wake Suha kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Akizungumza katika kipindi maalum cha Al-Jazeera, mkurugenzi wa kituo hicho cha utafiti, Francois Bochud, ameeleza kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina, walikuta chembechembe za polonium lakini amesema kwamba njia pekee ya kuthibitisha kuwa hata mwili wa Arafat ulikuwa na chembechembe za madini hayo ni kufukua maiti yake ili kuyafanyia uchunguzi zaidi. "Ni lazima tuchukue hatua za haraka kwani madini ya polonium yanaharibika hivyo tukisubiri kwa muda mrefu, ushahidi utapotea," alisema Bochud.
Ripoti za hospitali zaonyesha kwamba damu haikuwa na sumu
Madini ya polonium ndiyo yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa jasusi wa Urusi, Alexander Litvinenko, aliyeuwawa jijini London, Uingereza, mwaka 2006. Inaaminika kwamba Litvinenko aliuliwa kwa makusudi.
Lakini hivi sasa mjane huyo anataka maiti ya marehemu mumewe ifukuliwe ili ifanyiwe uchunguzi kama ilivyokuwa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik Hariri. "Tunapaswa kuchukua hatua moja zaidi na kuufukua mwili wa Yasser Arafat ili kudhihirisha ukweli kwa jumuiya yote ya kiislamu na ulimwengu wote wa Kiarabu," alisema Suha.
Arafat alifariki November mwaka 2004 katika hospitali ya kijeshi nje kidogo ya mji mkuu wa Ufaransa, Paris baada ya kupatwa na kiharusi.
Mwaka mmoja baadaye, gazeti la The New York Times la Marekani, lilipokea ripoti ya hospitali hiyo ya Ufaransa. Ripoti hiyo inaonyesha kwamba hapakuwa na chembechembe zozote za sumu katika damu ya Arafat.
Uvumi kwamba Arafat aliuliwa na Waisraeli umekuwepo kwa miaka minane sasa tangu kifo cha kiongozi huyo.
No comments:
Post a Comment