"Hali ya Nigeria bado ipo kwenye uchunguzi wa awali tu, na ikiwa kama tutaona kwamba matukio yale yale ya uhalifu ndiyo yanayoshughulikiwa na serikali ya Nigeria, basi hakutakuwa na haja ya ICC kuingilia kati." Bensouda aliwaambia waandishi wa habari mjini Abuja.
Bensouda amesema kwamba si lengo la Mahakama yake kuingilia mambo ya ndani ya Nigeria, licha ya kwamba matukio ya kigaidi yanayotokea yanaweza pia kufanana na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.
Rais Jonathan ataka mazungumzo na Boko Haram
Kufuatia mashambulizi mabaya kabisa ambayo yalisababisha vifo vya watu 185 katika mji wa Kano hapo Januari 20, Rais Jonathan aliwataka Boko Haram kuingia kwenye mazungumzo,Lakini rais huyo amemwambia Mwendesha Mashtaka wa ICC kuwa serikali yake haitatoa kinga ya kutoshitakiwa kwa makosa makubwa ya uhalifu.
Kwa miaka kadhaa pia, ICC imekuwa ikichunguza ghasia za kidini nchini Nigeria katika kile kinachoitwa "Mkanda wa Kati", ambao unaigawa jamii ya kusini yenye Wakristo wengi na ya kaskazini yenye Waislamu wengi.
No comments:
Post a Comment